Your Email*
Your Message
Δ
Tithi, Anu na Kushum hawahitaji mabawa ili kupuruka kama ndege au kereng'ende. Kupitia uwezo wa mchezo na mabawa ya kudhania, wanapuruka juu zaidi kama tiara au kundi la mawingu.
Putu ni samaki mdogo. Gutu ni samaki mkubwa mwenye meno makubwa! Hayaaa! Gutu anakuja kumkamata Putu? Putu atatorokaje?
Tumbili Mdogo na Samaki ni hadithi kuhusu tumbili mdogo mwerevu anayependa mchezo anayejifunza jinsi maisha duniani kwa kumuiga mama yake. Katika safari yake, lazima aamue iwapo atachukua hatua za kijasiri au la. Unafikiri atafanya nini?
Tembo anajaribu kumsaidia nyuki mdogo aliyepotea kupata mahali anapoishi. Je, ni kiota? Pango? Anaishi wapi?
Je, unaweza kutambua wanafamilia ambao ni warefu na wafupi? Kitabu hiki kinaonyesha dhana ya kinyume— refu na fupi— kupitia wanafamilia wa mtoto.
Panya anapenda kucheza mchezo wa kuruka miraba iliyochorwa ardhini lakini hana mtu wa kucheza naye. Jirani yake, Mbuzi, yuko nyumbani lakini anapenda kukaa peke yake. Je, Panya ataweza kumshawishi Mbuzi kucheza naye?
By navigating this website, you agree to the storing of cookies on your device to enhance site navigation and analyze site usage.