Watoto walioumbwa kwa nta
Palikuwa na familia moja ya watoto watatu watiifu. Ilikuwa shida kwani walikuwa watoto wa nta kwa hivyo walifanya shughuli zote usiku kwa kuhofia kuyeyushwa na jua kali. Lakini mvulana mmoja anatamani sana kuiona dunia mchana na hivyo anatoka na kutembea nje. Bila shaka, anayeyushwa na joto jingi la jua. Nduguze wanavunjika mioyo lakini wanapanga jinsi ya kumsaidia ndugu yao.